The House of Favourite Newspapers

Mtwara: Wanafunzi Wasomea Chini ya Mkorosho

0

WANAFUNZI  wa Shule ya Msingi Namalombe wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara pamoja na Mwalimu mkuu wao, Bwanaheri Akili, wameiomba serikali iwasaidie kuwajengea madarasa kwani kwa sasa wanapata shida kusomea chini ya mkorosho kama darasa baada ya shule yao kuwa na darasa moja tangu ilipoanzishwa mwaka 2014.

 

 

Mwalimu huyo amesema wanafunzi wa darasa la saba, la kwanza na awali wanalazimika kusoma chini ya mkorosho huku darasa pili, la tatu, la nne, la tano na darasa la sita wote wakisoma katika jengo la darasa moja lililopo na kufanya kiwango cha kufundisha kuwa kidogo huku wakitumia choo kimoja cha nyasi, walimu na wanafunzi.

 

 

 

Hayo yamebainika baada ya ziara ya Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde, alipofika shuleni hapo baada ya kupata taarifa  ya kuwepo kwa shule hiyo yenye darasa moja tu na kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara, Hamis Dambaya, ndani ya miezi miwili wajenge madarasa manne haraka na kutenga katika bajeti ujenzi wa nyumba za walimu, ofisi na madarasa mengine huku yeye akiahidi atawapelekea gharama za madarasa matatu kutoka ofisi ya Tamisemi.

 

Leave A Reply