The House of Favourite Newspapers

Muendelezo wa matukio katika tamasha la Majimaji Selebuka

0

Mabingwa wa mbio za wanawake katika Tamasha la Majimaji Selebuka. Kutoka kulia ni bingwa wa mbio za kilometa tano za wanawake, Neema Ndambo, Mwanaharabu Pili aliyeshika nafasi ya pili na mshindi wa tatu, Shakira Abdallah.

Mama na mwana….Bibie Abdallah kushoto akiwa katika pozi na mwanaye, Shakira Abdallah, wote walishiriki katika mbio za wanawake za Km 5, katika Tamasha la Majimaji Selebuka. Mama ameshika nafasi ya tano, mwana nafasi ya tatu.
Washindi wa mbio za wanawake katika picha ya pamoja na viongozi wa tamasha la Majimaji Selebuka 2015.
Washiriki wa mbio fupi za wanawake wakiwa wamepumzika baada ya kukimbia.
Shakira Abdallah akimalizia mbio katika shindano la mbio za wanawake Km 5 zilizoandaliwa na Asasi ya Somi katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015. Shakira ameshika nafasi ya tatu licha ya kukimbia peku.
Mkurugenzi mwenza wa Asasi ya Songea-Mississippi, Dk Damas Ndumbaro kulia akipata maelezo kutoka kwa wajasiriamali katika maonyesho ya wajasiriamali kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2015, kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, mjini Songea.
Mmoja wa askari barabarani akiwa na cheti alichotunukiwa katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.
Bingwa wa mbio za wanawake, Neema Ndambo akishangilia baada ya kuvishwa medali ya dhahabu na kupokea kitita cha fedha tasilim katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015
Wananchi mbalimbali wakipata ufafanuzi kutoka kwa wajasiriamali katika maonyesho ya bidhaa zao kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.
Washindi wa mbio za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa tamasha la majimaji selebuka.
Mkurugenzi mwenza wa Asasi ya Songea-Mississipi, Prof. Julian Murchison akipewa maelekezo na wajasiriamali katika maonyesho ya bidhaa zao kwenye tamasha la majimaji selebuka 2015.
Mshindi katika mdahalo wa Tamasha la Majimaji Selebuka Jonathan Patrick (katikati) kutoka shule ya Kigonsera High School, mshindi wa pili ni Mwajuma Hassan kushoto kwake wa Shule ya Sekondari ya Londoni na Godliving Bayona wa Kigonsera aliyeshika nafasi ya tatu.

(Habari/Picha: Nicodemus Jonus GPL, Songea)

 

Leave A Reply