The House of Favourite Newspapers

Mugabe Awaambia Wanajeshi Hatajiuzulu Urais

0
Robert Mugabe wa Zimbabwe.

RAIS Robert Mugabe wa  Zimbabwe ameripotiwa kukataa kuondoka madarakani licha ya kuongezeka kwa wito mbalimbali wa kumtaka ajiuzulu.

 

Mugabe, 93, aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka ipatayo 37,  amezuiliwa  nyumbani kwake wakati jeshi lilipochukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu  nani atakuwa mrithi wake.

Mugabe (wa pili kulia) ambaye amezuiwa nyumbani kwake, akiwa na mkuu wa majeshi, Constantino Chiwenga (kulia).

 

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa kati ya Muganbe na ujumbe kutoka nchi za kanda hiyo.  Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani.

Kiongozi wa upinzani,  Morgan Tsvangirai,  alisema kuwa kwa manufaa ya watu wa Zimbabwe, Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja.

 

Jeshi lilichukua hatua hiyo baada ya Rais Mugabe kumfukuza Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopiya, jambo lililoashiria kuwa alitaka nafasi hiyo ichukuliwe na  mkewe Grace Mugabe, ambapo angekuwa kiongozi wa chama cha Zanu-PF na  rais.

Mugabe akiwa na mkuu wa majeshi aliyeongoza majeshi dhidi yake.

Taarifa zilizopo zinasema Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980 anakataa kuondoka kwa hiari kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  mwaka ujao.

 

Baadhi ya wadadisi wa mambo wanasema  Mugabe anajaribu kujihakikishia usalama na familia yake kabla ya kuondoka madarakani.

 

Maafisa wa Zanu PF mapema walisema Mugabe atabakia madarakani hadi kufanyika mkutano mkuu wa chama hicho  mwezi Desemba wakati Mnangagwa atakiongoza chama na hatimaye kuwa rais.

NA WALUSANGA NDAKI | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply