The House of Favourite Newspapers

Mugabe: Alipambana na Wazungu, Akawaumiza Watu Wake! – Video

UKISIKIA watu wanasema tuko nyuma yako, uwe na tahadhari,  maana ukigeuka unaweza usiwakute. Hii inaonekana imetokea laivu kwa Robert Mugabe pale alipojitoa mhanga kubishana na walimwengu wengine kwa maslahi aliyoyajua mwenyewe, matokeo yake wananchi wake ndiyo wakaumia  kwa vikwazo vya uchumi na diplomasia walivyomwekea.

 

Viongozi wa Afrika wakamtelekeza, leo hii amekufa, viongozi wanashindana kumsifia Mugabe kwa mbwembwe na mikogo kwa sababu marehemu hatukanwi. Haya ndiyo maajabu makuu ya viongozi wa Afrika!

 

Tatizo la Afrika ukiwa wa misimamo ya aina yako, ujue utakabiliwa na tisho la kuuawa au kukwamishwa kisiasa kama walivyomkwamisha Nyerere na ujamaa wake,  Mugabe na misimamo yake.

SIKILIZA HAPA

Comments are closed.