Kartra

Mugalu Arejea Kuivaa Yanga

MSHAMBULIAJI wa Simba, raia wa DR Congo Chriss Mugalu, amerejea kuwavaa Yanga hii ni baada ya kukosa mechi mbili zilizopita kutokana na kuwa na maumivu ya msuli.

 

Mugalu ambaye mpaka sasa ana mabao 10 kwenye msimamo wa wafungaji bora Ligi Kuu Bara, aliumia mguu kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ulioisha kwa Simba kushinda bao 1-0.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe amesema kuwa: “Hali ya Mugalu ipo vizuri kwa sasa na ameanza mazoezi na wenzake, yupo katika hali nzuri na ni chaguzi ya kocha kutaka kumtumia.

 

“Kwa sasa hatuna majeruhi hata mmoja wachezaji wote wapo sawa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga.”Wikiendi hii, Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

STORI: CAREEN OSCAR,Dar es Salaam

MAGAZETI JULAI 02: RIPORT YA CAG NI KAA LA MOTO | RAIS SAMIA AWAGUSA WANANCHI WA VIJIJINI


Toa comment