The House of Favourite Newspapers

Mugalu Mtambo Wa Mabao, Unaoitisha Plateau United

0

“MECHI ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) tuliyocheza na Yanga Julai 12, mwaka huu tulitakiwa kupata ushindi mnono wa mabao zaidi ya 4-1 tulioupata, lakini kwa bahati mbaya washambuliaji wetu walishindwa kutumia nafasi walizokuwa wanazipata.

 

“Hiyo ndiyo sababu iliyonisababisha nifanye maamuzi ya kutafuta mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao ambaye ni Mugalu (Chris).

 

“Mugalu atasimama katikati na muda wote kazi yake itakuwa ni kufunga mabao tu,” hii ilikuwa nukuu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Waku rugenzi ya Simba, Moha mmed Dewji ‘MO’ akizun gumzia usajili wa straika wao mpya Mkon gomani, Chris Mugalu.

 

Mabosi wa Simba walichukua usafi ri kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiwa na kiasi cha Sh milioni 140 mkononi kuelekea Zambia kwa ajili ya Mugalu ambaye alikuwa anakipiga kwenye kikosi cha Lusaka Dynamos. Baada ya mazungumzo ya kina, pande hizo mbili zikakubaliana na straika huyo akamwaga wino wa miaka miwili kwenye timu hiyo.

 

Tangu ametua kikosini hapo, kabla ya majeraha Mugalu amegeuka silaha ya kocha, Sven Vandenbroeck kwenye suala zima la kufunga mabao. Ndani ya mechi nne ambazo Mugalu ameichezea Simba, ameifungia mabao matatu.

 

Nyota huyo amekosekana kwenye mechi nyingi kutokana na majeraha. Katika mechi 10 za ligi ambazo Simba imecheza, amekosekana kwenye mechi sita dhidi ya Ihefu, Mtibwa, Prisons, Ruvu Shooting, Kagera na Yanga.

 

Amecheza mechi nne za ligi, akifunga mfululizo katika mechi tatu dhidi ya Biashara, Gwambina na JKT Tanzania, mechi pekee ya ligi ambayo alicheza bila kufunga ni dhidi ya Mwadui. Baada ya kuivaa JKT, akacheza mchezo wa kirafi ki dhidi ya African Lyon akafunga mabao mawili kisha akaumia.

 

Hadi hapo, inaonyesha kuwa Mugalu ni hatari anapokuwa uwanjani. Lakini Simba imemsajili maalum kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambayo sasa imefi ka na inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

 

Simba imepangwa na Plateau ya Nigeria katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na staa huyo anafunguka malengo namna hii; “Lengo kubwa ambalo tunalo kwenye kombe hilo ni kutwaa ubingwa huo, kwa kupitia uwezo wangu na wengine naamini tutafanikisha jambo hilo.

 

“Nafahamu Simba wanataka kutwaa ubingwa wa kombe hilo, hivyo nitapambana kuonyesha uwezo nilionao. Wote hapa ni wachezaji wakubwa na kufi ka kwangu kutaifanya timu kwenda mbele katika mashindano hayo.

 

IPI IMEKUWA SIRI INAYOKUBEBA KATIKA KUFUNGA?

“Namshukuru Mungu kwa hali hii inayonikuta ya kufunga kila mechi, siri yangu ni kumuamini Mungu na kujiamini binafsi. Lakini siku zote mimi nimekuwa mtu mwenye uchu wa kufunga mabao niwapo uwanjani.

 

IKITOKEA HUFUNGI UNAKUWAJE?

“Nisipofunga najisikia vibaya sana, naona kama sijafanya kazi yangu vizuri, na inanipa deni la kuhakikisha napambana kwenye mechi nyingine ili niweze kufunga, kwani lengo ni kuifanya timu ipate matokeo mazuri katika kila mechi.

 

UHUSIANO WAKO NA BOCCO, KAGERE UKOJE?

“Kwangu upo vizuri, na ndiyo maana nimekuwa tayari kucheza na mtu yeyote yule ambaye kocha anaamua kunianzisha naye kwenye eneo la ushambuliaji. “Wote Kagere na Bocco, wana uwezo mzuri na mkubwa na ninashirikiana nao vizuri kabisa bila ya shida kwa sababu lengo letu kwa pamoja ni kushinda.

 

UNAWAZUNGUMZIAJE MABEKI WA BONGO?

“Mara zote ambazo napambana nao inakuwa vita kwa sababu wao wanalinda na sisi tunataka kushinda. Unajua Simba ni timu kubwa hivyo kila timu tunapocheza nayo inajitahidi kupambana ili watuzuie tusiweze kufunga, lakini na sisi tunapambana kufanya vizuri.

 

MKIANZISHWA WOTE NA KAGERE, BOCCO ITAKUWAJE?

“Tukipangwa wote tunakuwa na nia moja tu ya kuifanya Simba itimize kile ambacho inakihitaji ambacho ni pointi tatu. Tutapambana kwa ajili ya kutimiza malengo ya timu kwenye kila mechi.

 

NINI KIMEKUFURAHISHA TANGU UTUE TANZANIA?

“Kupokelewa vizuri na mashabiki wa hapa na kuonyesha hali ya kunifurahia, hilo lilinifurahisha sana baada tu ya kuwasili na linanifanya nipambane kwenye mechi zote.

 

REKODI YA MABAO YA JUU KUFUNGWA HAPA NI 26, KWAKO UNAWEZA KUIVUNJA?

“Kuhusu kuivunja rekodi hiyo ya mabao inawezekana kabisa endapo tu kocha (Sven) ataendelea kunipatia nafasi ya kucheza mara kwa mara. “Nikiwa na uhakika wa kucheza basi siyo jambo gumu sana kufi kia idadi hiyo ya mabao kwa sababu naamini ninaweza kufunga katika kila nafasi ambayo nitapata.

Rekodi hiyo ya mabao 26 inashikiliwa na straika wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ aliyeiweka msimu wa 1999. Kwa sasa Mugalu ana mabao matatu baada ya kucheza mechi nne.

 

UNAWAAHIDI NINI MASHABIKI WENU?

“Tuko hapa kwa ajili ya kuwapa furaha hivyo tutapambana kuwapa kile ambacho wanakitaka kutoka kwetu. Tutapambana kuwapa furaha mara zote.

 

KWA UJUMLA UNAWAONAJE WACHEZAJI WENZAKO?

“Simba ina wachezaji wakubwa na kikosi kizuri kwa ujumla, namfurahia kila mchezaji ambaye niko naye hapa ndani ya kikosi. Ushirikiano wetu ndio utatufanya tufanye vizuri msimu huu.

 

HIVI KABLA HUJAJA SIMBA ULIIFAHAMU?

“Ndiyo. Simba ni timu kubwa nilikuwa naifahamu kabla ya kuja kwa sababu nilikuwa naifuatilia katika mitandao. Lakini hata wakati wananitaka nilijisikia vizuri sababu wachezaji wanaokuja hapa ni wakubwa na wana mashabiki wengi.

 

UGUMU GANI UNAKUTANA NAO LIGI KUU BARA?

“Kitu kimoja ni kwamba tukiwa wazima na tukiwa pamoja, hakuna ugumu wowote ule tunaokutana nao kwa sababu tunashirikiana nao, hiyo inatupa nafasi ya kushinda mechi zetu za aina yoyote,” anamaliza Mkongomani huyo ambaye hivi karibuni amerejea uwanjani akitokea kwenye majeraha.

SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave A Reply