Mukoko Aleta Jembe la Maana Yanga

KAMA mambo yakienda sawa, basi usishangae kuona Yanga wakimshusha beki Ousmane Adama Ouattara raia wa Ivory Coast ambaye anakipiga kwenye kikosi cha AS Vita ya DR Congo.

 

Beki huyo wa kati, anaweza kushuka Jangwani baada ya mabosi wa kikosi hicho kupewa mchongo na kiungo wao, Mukoko Tonombe kwamba kama wakimpata atawasaidia sana kwenye safu ya ulinzi ambayo kwa sasa inaongozwa na Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto.

 

Ouattara ambaye thamani yake inatajwa kuwa ni euro 250,000 (sawa na Sh 706.7m za Kitanzania), mkataba wake wa sasa unatarajia kumalizika Juni mwakani.

 

Habari ambazo Spoti Xtra, limezipata ni kuwa, beki huyo anaweza kumwaga saini Yanga kutokana na mabosi wa Jangwani kuona faida ya wachezaji ambao wamewasajili kutoka AS Vita.“

Huyo beki anaweza kuja kwa sababu wameambiwa na wachezaji ambao wametoka AS Vita kwamba anaweza kufanya kazi na kuifanya Yanga kuwa na ukuta mgumu zaidi ya uliopo sasa.“

 

Uzuri ni kuwa wao wenyewe wameona wachezaji wote ambao wamesajiliwa kutoka klabu hiyo nini ambacho wamekifanya na mipango hiyo inafanyika kwa sasa japokuwa kwa siri.“

 

Kwa sasa kitu ambacho kitazuia dili hilo kutokamilika kwa wakati ni dau kubwa la mchezaji mwenyewe lakini nje ya hapo basi hakuna kipingamizi kingine ambacho kinaweza kumfanya asije,” kilisema chanzo hicho.

VIBE ya MASHABIKI wa YANGA Baada ya KUWAFUNGA IHEFU – “WACHEZAJI Wakiharibu, TUSIPANIKI”

Toa comment