The House of Favourite Newspapers

Mukoko Atangaza Vita Yanga

0

KIUNGO wa Yanga raia wa DR Congo, Mukoko Tonombe, ameahidi kufanya mazoezi mazito ili aweze kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

 

Mukoko msimu huu amekuwa na wakati mgumu wa kucheza kikosi cha kwanza kutokana na kupata upinzani mkali mbele ya Mganda, Khalid Aucho.

 

Katika mechi tano za Ligi Kuu Bara msimu huu, Mukoko amecheza moja, huku Aucho akicheza nne ambapo Kocha Nasreddine Nabi, eneo la kiungo amekuwa akiwatumia zaidi Yanick Bangala, Feisal Salum na Aucho, huku Zawadi Mauya na Mukoko wakisubiri.

 


Akizungumza na Spoti
Xtra, Mukoko amesema: “Natamani sana ligi ikiendelea nipate nafasi ya kucheza ili nifanikishe lengo langu la kuchukua Tuzo ya Mchezaji Bora msimu huu.“Nitajitahidi kufanya mazoezi makali ili tu niweze kupata nafasi mbele ya viungo wenzangu ambao kwa sasa wanaaminiwa na kocha.”

STORI: MUSA MATEJA, DAR ES SALAAM

Leave A Reply