Kartra

Mukoko Awaangukia Yanga “Sikukusudia”

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Mukoko Tonombe kupitia ukurasa wake wa Instagram amewaomba radhi mashabiki pamoja na benchi la ufundi kwa kile kilichotokea jana kwenye mchezo wa fainali kati ya @simbasctanzania na @yangasc baada ya kulimwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu nahodha wa Simba John Bocco.

Kupitia Instagram yake ameandika kuwa: “Nachukuwa fursa hii kuomba radhi mashabiki pamoja na viongozi na benchi la ufundi kwa kilicho tokea katika mchezo wa fainali wa Yanga vs Simba. Kwamba sijakusudia kupewa kadi nyekundu ambayo labda ndio ilikuwa sababu ya kupoteza mchezo huo. Naipenda sana team yangu Yanga DAIMA MBELE NYUMA MWIKO💚🧡.


Toa comment