The House of Favourite Newspapers

Mukoko: Nitamiss Ugali na Samaki

0

Baada ya kuthibitishwa ameondoka Young Africans na kusajiliwa TP Mazembe ya nchini kwao DR Congo, Kiungo Mkabaji Mukoko Tomombe ametoa ya moyoni.

Mukoko ameondoka Young Africans akisisitiza kuipenda klabu hiyo iliyomsajili mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea AS Vita ya ya mjini Kinshasa-DR Congo.

 

Kiungo huyo amesema daima klabu hiyo Kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itaendelea kubaki moyoni mwake, kufuatia maisha mazuri aliyoishi klabuni hapo.

Amesema aliishi vizuri na wachezaji wenzake, viongozi, mashabiki na wanachama, hivyo alijihisi yupo nyumbani katika kipindi chote alichokaa Young Africans.

 

Maneno hayo ya mapenzi ya dhati kwa Mukoko dhidi ya Young Africans, ameyaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram usiku wa kuamkia leo, ambapo dili lake la kuondoka Young Africans lilishika hatamu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

 

“Yanga ni kama familia kwangu. Siku zote itabaki moyoni. Nitaikumbuka Tanzania hasa kwa ugali na samaki wa baharini.“ Teacher Mukoko Tonombe.

 

Mukoko amelazimika kuondoka Young Africans, kufuatia kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza, baada ya kusajiliwa kwa viungo Khalid Aucho na Yanick Litombo Bangala msimu huu 2021/22.

Dili lake la kwenda TP Mazembe limechagizwa na usajili wa Chiko Ushindi Wakubanza aliyetokea klabu hiyo ya Lubumbashi hadi Young Africans, wakati wa Dirisha Dogo la Usajili lililofungwa rasmi Januari 15.

Leave A Reply