The House of Favourite Newspapers

Mukoko, Waziri Junior ‘Waizamisha’ Mlandege 2-0 Chamanzi

0

TIMU ya yanga  Septemba 16, 2020 imecheza mechi  ya kirafiki  katika dimba la Azam Complex Chamazi ambapo   dhidi ya Mlandege FC ya Zanzibar.

 

Yanga imeshinda mabao 2-0, la kwanza limewekwa wavuni na Waziri Junior kwa mkwaju wa penalti dakika ya 40 na la pili limefungwa na Mukoko Tonombe aliyepiga shuti kali nje ya boksi lililoenda kwenye wavu na kumshinda kipa wa Mlandege dakika ya 59 baasa ya klutengewa mpira na Sogne.

Yanga walitumia vikosi viwili tofauti kwa vipindi viwili walicheza mpira wa kuumiliki na kuanzisha mashambulizi kutokea pembeni.

 

Kikosi kilichoanza Yanga kabla ya mabadiliko golini alikuwa Metacha Mnata, mabeki Kibwana Shomari, Adeyun Salehe, Said Makapu, Abdallah Ninja, viungo Fei toto, Abdulaziz Makame, Farid Mussa, Haruna Niyonzima, washambuliaji Ditram Nchimbi na Waziri Junior.

Wachezaji walioingia kipindi cha pili walibadilisha mchezo wakiongozwa na Deus Kaseke, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong, Carlos Carlinhos na Zawadi Mauya huku langoni akiingia Ramdhan Kabwili.

Raundi ya tatu ya Ligi Kuu Bata itaendelea wikiendi hii na Azam FC itasafiri kwenda Mbeya kucheza na Mbeya City jijini huku Yanga ikitua Bukoba kukipiga na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba.

Leave A Reply