The House of Favourite Newspapers

MultiChoice Yatangaza Washindi Wa Mafunzo ya Filamu Nairobi

Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, ndugu Alpha Mria akielezea kwa undani namna mchakato huu wa kupata vijana wenye vipaji na mapenzi kwenye sekta ya Filamu na mwisho kupatikana washindi hawa wane ambao mnamo Octoba 2018 wataenda kuiwakilisha Tanzania kwenye ya Mafunzo Maalum ya Tasnia ya Filamu MultiChoice Talent Fatory, huko Jijini Nairobi Kenya kwa kipindi cha mwaka mzima.

MultiChoice Tanzania, Imetangaza  washindi  wanne waliokidhi vigezo katika shindano la MultiChoice Talent Factory lilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka huu.

 

Programu hii itawezesha jumla ya vijana 60 kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika kuweza kupata mafunzo ya filamu kwa kipindi cha mwaka mmoja katika vituo vitatu tofauti, kimojawapo kikiwa nchini Kenya (Nairobi) ambapo vijana hawa watakuwapo ifikapo tarehe 01 Oktoba mwaka huu.

 

Mchakato mzima  wa kupatakana kwa washindi hawa ulichukua takribani muda wa miezi miwili ambapo kwa hapa nyumbani Tanzania tulipokea maombi kutoka kwa vijana zaidi ya 160, yaliyofuatiwa na mchujo ulifanyika tarehe 20 Julai Mwaka huu hapa Dar es Salaam Tanzania.

Picha ya Pamoja ya Uongozi wa Multichoice Tanzania wakiwa na Vijana walioibuka kidededea watakao kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Mafunzo Maalum ya Filamu Multichoice Talet Factory, jijini Nairobi Kenya, kutoka kusho ni Jamal Kishuri kutokea Arusha, Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, katikati ni Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifuatiwa na mshindi Sarah Kimario kutokea Dar es Salaam, pembeni ni Menejea Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria na mwisho kulia ni mshindi wetu mwingine Wilson Nkya kutoka Kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa halfa hiyo.

“Maendeleo ya nchi yetu kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi tulizonazo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori, na kadhalika huku sekta ya ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo sekta ya sanaa na ubunifu kuwa na mchango mdogo katika ukuaji wa uchumi wetu.

 

Ili kuhakikisha kuwa tunasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya mihimili ya uchumi wetu, MultiChoice imeanzisha program hii na tumeanza na sekta ya filamu. Vijana wa kitanzania waliofanikiwa kufudhu katika mchakato huu ni Sarah Kimario  kutokea Dar es Salaam, Wilson  Nkya kutoka Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, alisema Alpha Mria  Meneja Masoko MultiChoice Tanzania.

Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo pamoja na Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria wakiwapongeza vijana hawa wakitanzania walioibuka washindi wa mpango huu wa kukuza tasnia ya Filamu Afrika unaotambulika kama Multichoice Talent Factory, vijana hawa wataliwakilisha Taifa kwenye mauzo haya maalum ya mwaka mzima yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya, kwa ukanda wa Afrika Mashariki yakiwa yameandaliwa na kugharamiwa na MultiChoice Afrika.

Tumebarikiwa kwa vipaji vingi katika fani mbalimbali na bila shaka tukiwekeza katika vipaji vya vijana wetu bila shaka tutafanikiwa kupanua wigo wa ajira na uchumi wetu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Amesema mafunzo hayo yataanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu itawawezesha vijana hawa wanne kutoka Tanzania kuungana na vijana wengine kutoka nchi mbali mbali za Afrika katika vyuo maalum vya mafunzo ya utengenezaji wa filamu ambavyo vitakuwa nchini Nigeria, Kenya na Zambia.

 

Kwa upande wao, washindi waliotangazwa kufudhu katika program hii wametoa shukrani zao za dhati hususani kwa kampuni ya MultiChoice sambamba na serikali ya Tanzania kwa ujumla. Akiongea katika hafla nhiyo, Wilson Nkya mmoja kati ya vijana waliopata fursa hiyo alisema kuwa “ Kipekee hii ni fursa tuliyokuwa tukiisubiri kwa muda mrefu na tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Kampuni ya MultiChoice, serikali na jamii yote kwa ujumla.  Tunaahidi kufanya kila liwezekanalo na mtegemee matokeo chanya kutoka kwetu’, alimalizia Wilson.

Kwa ufupi;

  • Mafuzo rasmi kuanza mwezi wa Oktoba 2018, jijini Nairobi, Kenya
  • Maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti ya www.multichoicetalentfactory.com
  • Washindi waliochachaguliwa ni wanne (4)
  • Gharama zote zitalipiwa na MultiChoice kwa kipindi cha mwaka mmoja

Tembelea ulingo wa MTF Mitandaoni kwa  #multichoicetalentfactory kwa taarifa Zaidi:

  • Instagram: @multichoicetalentfactory;
  • Twitter: @MCTalentFactory
  • Facebook: @multichoiceafricatalentfactory

 

Comments are closed.