Mume Adaiwa Kumuua Mkewe Kisa Kunyimwa Unyumba – Video
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma linamsaka Martin Hyera kwa kosa la kumuua mke wake Luciana Kapinga kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani chanzo kikiwa kunyimwa unyumba.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma SACP Marco Chilya amesema kuwa, mnamo Novemba 14, 2024 Majira ya saa 12 asubuhi katika kitongoji cha Mbilo kijiji cha Kizuka kilichopo Kata ya Kizuka Tarafa ya Mhukuru Wilayani Songea, mwanamke aliyejulikana kwa jina la Luciana Dastani Kapinga (22) mkulima mkazi wa Kitongoji cha Mbilo aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito chenye ncha kali maeneo ya kichwani upande wa juu wa jicho la kushoto hadi kichwa kubonyea na mume wake aitwaye Martin Hyera baada ya kumnyima unyumba.
“Wawili hao walionekana alfajiri wakikimbizana huku Mtuhumiwa Martin Hyera akiwa ameshika mpini wa Shoka kisha kutekeleza Mauaji hayo na baada ya kutekeleza mtuhumiwa alimpigia simu shangazi yake aitwaye Paulina Nchimbi na kumjulisha kuwa amemuua mke wake kwa sababu amekuwa akimnyima unyumba kwa muda mrefu kisha mtuhumiwa huyo alitorokana anatafutwa na polisi”.