The House of Favourite Newspapers

Mume Amuua Mkewe Kwa Kumng’oa Kidevu na Kumpiga kwa Kitu Kizito Kichwani

0
Masanja Mathias, Baba wa Mwanamke

MWANAUME Mmoja Aliejulikana kwa Jina la Edward Francis, (20) mkazi wa kijiji Cha Nyabugela Kata ya Mganza wilayani Chato Mkoani Geita, amedaiwa kumuua mke wake, Mariam Masanja, kwa kumng’ata kidevu na kumpiga na kitu kizito eneo la kichwa mpaka kumsababishia Umauti.

 

Tukio hilo limetokea mapema wiki hii ambapo mwanaume huyo anadaiwa kwenda nyumbani kwao na marehemu kuhani msiba wa shemeji yake ambaye alikua ni Kaka wa Marehemu.

Eneo la tukio yalipofanyika mauaji

Wazazi Pamoja na shuhuda wa tukio hilo wanasema Edward alifika nyumbani hapo kutoa pole ya msiba baada ya kutoka Mahabusu kwa dhamana ndipo alipomkuta mke wake na kumbeba kwenda Kurekebisha tofauti ambazo walikua nazo zilizo msababishia mwanamke kukimbia mji Kabla ya yeye kwenda Mahabusu.

 

Inasemekana baada ya wawili hao kuondoka nyumbani kwao na marehemu na kwenda nyumbani walipokua wakiishi, Usiku wa siku hiyo ndipo likatokea tukio hilo, inadaiwa baada ya tukio hilo Edward na familia yake walikimbilia kusiko julikana huku Dada wa mwanaume huyo akikimbia na mtoto.

Leave A Reply