Mume Amwekea Pilipili, Aziba na Gundi Nyeti za Mkewe – Video

POLISI katika Kaunti ya Taraka Nithi nchini kenya, wanamshikilia mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la James Muriuki, kwa tuhuma za kumwekea mke wake pilipili kwenye sehemu zake za siri na kisha kumziba na gundi.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 21, 2020, na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini humo, imeeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa akiwa mafichoni katika Kaunti ya Kitui, alipotorokea baada ya kutekeleza uhayawani huo.

 

Imeelezwa kuwa tukio hilo alilitekeleza Mei 16 mwaka huu, ambapo mke wake huyo aliokolewa na majirani waliompeleka hospitalini akiwa na hali mbaya.

 

Ofisi ya DCI imesema kuwa James Muriuki aliweka pilipili na chumvi, katika nyeti za mke wake huyo kwa kutumia kisu, kabla ya kumziba na gundi, ambapo mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Toa comment