MUME WA AMBER RUTTY AIBUKA!

SIKU chache baada ya Abubakary Milenga, baba mzazi wa msanii aliyetikisa kwa skendo ya video ya ulawiti, Nascat Abubakar ‘Amber Rutty’, kuibuka na kufunguka mazito yamhusuyo binti yake, kijana aliyekuwa mume wa msanii huyo aitwaye Rajabu Ally naye ameibuka na kusimulia mapya zaidi ikiwemo jinsi alivyochanganyikiwa alipoiona video chafu ya mkewe huyo.  Rajabu alifunga ndoa na Amber Rutty mwaka 2009 na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili; Shidadi na Mohamed.

AANZA KUFUNGUKA

Akielezea alipotoka na Amber Rutty ambaye jina lake kamili kwa mujibu wa baba yake mzazi ni Nascat, mume huyo alisema kuwa alifunga ndoa ya Kiislam na msanii huyo mwaka 2009 katika Kijiji cha Bomba-Mbili Mkoa wa Ruvuma.

“Amber Rutty alikuwa ni msichana mwenye maadili mazuri na hata mimi nilipomuoa nilijua wazi nimeoa mke mwenye maadili mema sana kwani alikuwa haachi kuswali hata siku moja na ni ngumu kuona kichwa chake kikiwa wazi bila kuwa na hijabu,” alisema mume huyo.

WAHAMIA DAR

Mume huyo alizidi kufunguka kuwa, mwaka 2012, walihamia jijini Dar kwa ajili ya kazi za ujenzi alizokuwa akifanya hivyo waliishi Mbagala-Kuu na maisha yakawa mazuri huku mkewe huyo akiendelea kuwa mwenye maadili mazuri na mama bora kwa watoto wake wawili ambao amezaa naye.

“Tuliendelea kuishi vizuri sana na nilikuwa nikimpongeza mke wangu kwa kupenda kuswali kila wakati na kufunga zote kila Ramadhani bila kuacha na mimi nilikuwa ninamuombea kwa Mungu, asibadilike, aendelee kuwa mke mwema mpaka tukapotenganishwa na Mwenyezi Mungu,” alisema Rajabu.

MAMBO YALIVYOANZA KUVURUGIKA

Akizungumzia siku mambo yalivyoanza kuharibika, Rajabu alisema mkewe alikuwa akipenda mambo ya saluni hivyo siku hiyo alimfuata na kumuambia kuwa karibu na mtaa wanaoishi kuna saluni hivyo alipenda awepo hapo kwa ajili ya kujifunza masuala ya saluni. Alisema hakuwa na kipingamizi, alimuomba amuite huyo mwenye saluni na kumpa masharti anayoyataka kabla ya mkewe huyo kuanza kujifunza kazi hiyo ya saluni.

“Sikumkatalia wazo lake kwa sababu nilijua ni vyema kujishugulisha hivyo nilivyomuita huyo mwenye saluni, nikampa masharti kwamba, kwa kuwa Amber Rutty alikuwa na watoto, anahitajika atoke saluni mapema na kuwahudumia na hata atakapoondoka awaache akiwa amewaandalia mahitaji yao ili wasipate shida,” alisema Rajabu.

Aliendelea kuweka wazi kuwa, baada ya kumkubalia alianza kwenda saluni hapo, lakini baada ya wiki moja mambo yalibadilika kwani alianza kurudi usiku wa saa nne na huku watoto wake wakiwa hawajala.

MAMBO YATIBUKA ZAIDI

Aliendelea kusema kuwa, mambo yaliharibika zaidi baada siku moja kurudi nyumbani kwake majira ya saa tatu usiku, lakini mkewe huyo hakuwa amerudi na watoto hawajala chochote, ikabidi aondoke nao mpaka pale saluni na kukuta pamefungwa. Alisema alijaribu kupiga simu yake ikawa haipatikani hivyo aliamua kurudi nyumbani na kuwanunulia watoto wake chipsi wakala, wakalala.

“Niliumia sana kuona watoto wangu wamejilaza bila kula wala kuoga hivyo niliwahudumia na kuwapa chakula, baada ya muda alikuja na nilipomuuliza hakuwa ananijibu vizuri niliachana naye na kumwambia sitaki tena kumuona anaenda pale saluni na nilimueleza huyo bosi wake pia,” alisema. Rajabu alisema baada ya kumkataza kila kukicha Amber Rutty akawa analeta visa visivyokuwa na kichwa wala miguu ambapo nyumbani akawa hakai, kutwa anatanga na njia.

Alisema alilazimika kuwakabidhi watoto kwa mama mwenye nyumba wake baada ya kuona mkewe hatulii nyumbani na yeye akasafiri kikazi, lakini alipokuwa huko safarini, alisikia kuwa Amber Rutty amechukua kila kitu ndani ameondoka na watoto kawaacha hapo. “Nilivyokuwa safarini Amber Rutty alichukua kila kitu ndani mpaka kijiko na kwenda kwa mwanaume ambaye anamsumbua na nilivyopata taarifa nilimpigia tukutane pale nyumbani na kuamua kumpa talaka na kumsihi nimrudishe nyumbani nilipomtoa akakataa.

“Akaondoka na kuniachia watoto wadogo ambapo mmoja alikuwa ana umri wa miaka miwili na mwingine minne, ilikuwa mwaka 2015,” alisema Rajabu.

AOMBA MSAMAHA

Rajab aliendelea kufunguka kuwa, baada ya wiki mbili tu kupita, msanii huyo alimpigia simu na kumuomba msamaha na kwa kumwambia kuwa amejifunza hivyo anaomba kurudi walee watoto.

“Baada ya kuniambia hivyo nilikubali, lakini aliniambia kuwa hataki kurudi tena pale tulipokuwa tukiishi hivyo nimtumie hela atafute chumba tulipe miezi mitatu ambapo nilifanya hivyo na kutuma elfu tisini manaa nilikuwa safarini, lakini baada ya hapo sikumpata tena,” alisema Rajabu.

AMBER AMZUIA MTOTO

Mume huyo alizidi kuweka wazi kuwa, baada ya kuomba hifadhi ya watoto wake, baadaye aliwahamishia kwa mwanamke wake mwingine na ndipo Amber Rutty alipoanza tabia ya kumzuia mtoto wake mmoja (Shadida) asiende shule. Alisema mtoto huyo aliyekuwa akisoma Shule ya Mbagala- Zakhem, Amber Rutty alikuwa akimvizia kituoni kila siku muda wa kwenda shule na kwenda naye nyumbani kwake anapoishi takriban mwezi mmoja.

“Nilimbana mtoto wangu wakati nimerudi safari kwa nini hajafika shule mwezi mzima ambapo aliniambia kuwa mama yake alikuwa akimchukua kila siku asubuhi wakati anaenda shule na kuamuachia muda wa mchana. Niliumia sana kwa sababu hata tabia ya mtoto wangu ilianza kubadilika,” alisema Rajabu.

Alisema kwa kuwa kipindi hicho yeye alikuwa na safari nyingine, alimuomba mwanamke aliyekuwa anaishi naye wakati huo aende mpaka shuleni hapo akamkabidhi Amber Rutty mtoto huyo mbele ya mwalimu mkuu shuleni hapo ili aendelee kukaa naye yeye mpaka akirudi ili kama akipata matatizo asiwe mikononi mwa mwanamke wake huyo mpya.

“Niliumia sana, nikaona bora nimwambie mwanamke wangu mpya ambaye natarajia kumuoa hivi karibuni amkabidhi mtoto huyo mbele ya mwalimu mkuu ili mimi nibaki na mmoja, lakini alishindwa kufanya hivyo kwa sababu mtoto alikataa kuondoka na mama yake huyo hivyo mpaka sasa naishi na wanangu wote wawili mwenyewe,” alisema Rajabu.

AMPOTEZEA MAZIMA

Mume huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kuona hamulewi mkewe huyo aliamua kumpotezea hadi siku alipoelezwa kuhusu video yake chafu.

“Siku hiyo nilikuwa kazini, yaani baada ya kuangalia hiyo video na kuona ni ya mama watoto wangu sikuongea chochote, niliondoka kimyakimya. Sikuweza kuendelea kabisa maana nilihisi akili yangu haikuwa sawa kabisa maana sikujua ni kitu gani kimempata Nascat (Amber), naumia sana kwa ajili ya watoto wangu maana walikuwa na mama mzuri sana,” alimaliza Rajabu. Amber Rutty bado yupo mahabusu baada ya kupandishwa kizimbani kwa kosa hilo katika Mahakama ya Hakimu

Toa comment