The House of Favourite Newspapers

Mume wa Mtu afanya Mambo ya Aibu!

0

Richard Bukos

Mwanaume mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja aliyedaiwa kuwa ni mume wa mtu, hivi karibuni alifanya mambo ya aibu ikiwemo kuvua nguo na kukata mauno mbele za wasichana.

Baba huyo akisakata rumba.

Tukio hilo lilijiri ndani ya Ukumbi wa Highway Night Park uliopo Ukonga jijini Dar wakati Bendi ya Mashujaa Musica ilipokuwa ikiporomosha burudani.Awali, mwanaume huyo ambaye ilidaiwa siku nyingine katika kiwanja hicho akiwa na ‘my wife’ wake alianza kupandwa na midadi kufuatia muziki uliokuwa ukipigwa, ikafika wakati akaamua kulivamia jukwaa na kuanza kuvua tisheti.

Baada ya kufanya hivyo, alipiga magoti staili ya mugongomugongo na kuanza kukatika, jambo lililowafanya baadhi ya watu waliokuwa eneo hilo waanze kumjadili.“Hii ni aibu, mtu mzima na akili zako huwezi kucheza staili zile tena mbele ya wasichana! Hivi ndugu zake au watoto wakiona picha zake itakuwa aibu ya aina gani?” alihoji mdau mmoja aliyekuwa ukumbini hapo.

Leave A Reply