The House of Favourite Newspapers

ads

Mume wa Osinachi Alijificha Kwenye Kivuli cha Uinjilisti

0
Mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu akiwa mahakamani

MAMA wa aliyekuwa mwimbaji wa Injili nchini Nigeria, Osinachi Nwachukwu ameiambia Mahakama kile kilichotokea kwa binti yake wakati wa maisha yake ya ndoa na Peter Nwachukwu kabla hajafa.

 

Mume wa marehemu Osinachi alimnyanyasa binti yake na kusababisha kifo chake, Caroline Madu ameiambia Mahakama Kuu ya Abuja.

 

Kifo cha Osinachi Nwachukwu kilichotokea Aprili 2022 na kuzua ghadhabu kote nchini Nigeria baada ya familia yake kudai kuwa alikabiliwa na ukatili wa majumbani kupitia mikono ya mume wake.

Marehemu Osinachi akiwa na mumewe

Mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu anakabiliwa na mashtaka 23 kuhusiana na mauaji ya bila kukusudia yaliyosababisha kifo cha Osnachi.

 

Madam Madu ndiye shahidi mkuu katika kesi ya Nwachukwu, mume wa marehemu Osnachi.

 

Mama wa Osinachi aliangua kilio wakati akisimulia jinsi Peter alivyokwenda nyumbani kwake akijificha kwenye kivuli cha mwinjilisti.

Marehemu Osinachi akiwa na familia enzi za uhai wake

Madu anasema tangu Osnachi aolewe kwa miaka 14, alirudi nyumbani kwake akiwa mgonjwa.

 

Mama huyo alitoa ushahidi mbele ya mahakama akisema Peter hakumruhusu kumtembelea binti yake kwa sababu anamwita mchawi.

 

Pia hakumruhusu mwimbaji marehemu Osinachi kuchangamana na ndugu yake yeyote.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply