visa

MUNA AFUNGUKA MADAI YA KUTOKA NA MBASHA!

Baada ya kudaiwa kutoka kimapenzi na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha, mwanamuziki Rose alphonce ‘Muna Love’ kwa mara ya kwanza ameibuka na kukanusha.  Akizungumza na amani hivi karibuni, Muna alisema kamwe hawezi kutembea na Mbasha kwa kuwa jamaa huyo anamchukuliakama kaka yake.

“Naanzaje mimi kutoka na Mbasha, sijui kwa nini watu wameanza kutufikiria vibaya, labda niwatoe tu hofu kwamba mimi na Mbasha ni marafiki wa muda mrefu sana na kama ni mfuatiliaji mzuri wa mambo yangu utagundua kwamba hata katika baadhi ya safari zangu huko nyuma nimewahi kuambatana naye, sema ni vile tu tulikuwa hatujaanza kupostiana, lakini watu wameanza kuongea hivyo baada ya sisi kuanza kupostiana kisha kutaniana mambo ya kawaida tu ndio wakaanza kufikiria tofauti,” alisema Muna.

 
Toa comment