MUNA akana kutumia ulokole kuibia watu
BAADA ya madai kuzagaa kuwa anatapeli, msanii wa filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna Love’ amekana kuwa hatumii kivuli cha ulokole alionao kuibia watu kama watu wanavyosema.
Akibonga na Amani baada ya habari kuzagaa mitandaoni kwamba amekuwa akitumiwa pesa na watu ili awaletee mizigo yao lakini mwisho analeta visingizio, Muna alisema kwamba watu wanashindwa kuwa waelewa kwani kuna muda anakuwa amepatwa na matatizo lakini siyo kweli kwamba huwa hawaletei mizigo yao.
“Sijui kwa nini watu hawapendi kuona maendeleo ya wenzao, hizo taarifa siyo za kweli ila ni kundi la watu wachache ambao wanataka kunichafulia jina, lakini kwa uwezo wa Mungu naamini hawataweza, hao wanaosema nimewadhulumu siyo kweli maana kila mtu aliyenitumia pesa ya mzigo nimempatia mzigo wake,” alisema Muna.
Stori: Memorise Richard