The House of Favourite Newspapers

MUNA ALIA NA WATOTO HAWA

Rose Alphonce ‘Muna Love’

MIEZI kadhaa baada ya mwanadada Rose Alphonce ‘Muna Love’ afiwe na mwanaye Patrick Peter, ameamua kumuenzi mwanaye huyo kwa kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watoto wenye matatizo.

Muna aliwahi kueleza kuwa, wakati mwanaye alipokuwa hai alikuwa na ndoto za kuja kuwa-saidia wenzake lakini ameondoka duniani bila kuitimiza hivyo atafanya kwa ajili yake.

Inaelezwa kuwa, Muna sasa hivi siyo yule ambaye watu walikuwa wakimchukulia, amemrudia Mungu na anafanya mambo makubwa kwa jamii ambayo mastaa wengi Bongo hawakuwahi kuwaza kuyafanya.

Uwazi lilifanya jitihada za kumtafuta Muna ili kuzun-gumzia kile anachokifanya kwa sasa na alipopatikana mahojiano yalikuwa hivi;

UWAZI: Unacho-kifanya sasa hivi, hujawahi kukifanya miaka ya nyuma, ni kwa nini leo na si jana?

Muna: Mwanangu Patrick alipokuwa hai, alikuwa akipenda kuwasaidia watoto wenzake na alikuwa akiniambia kuwa, akiwa mkubwa atasaidia wengine zaidi ya vile alivyokuwa anasaidia.

Alionekana kuguswa na matatizo ya watoto wenzake, sasa amefariki, naona moyo unanisukuma kufanya haya kwa niaba yake na naamini Mungu atanisimamia.

UWAZI: Unachokifanya siyo kitu kidogo, kinahitaji muda na pesa pia kuwasaidia hasa hawa watoto, ni nani yuko nyuma ya huu mpango?

Muna: Kwa kweli kuna baadhi ya vitu watu wananipa sapoti maana unajua watoto wengi wana uhitaji tofauti.

UWAZI: Kwa hiki unachofanya, kuna msanii yoyote ameguswa na labda akaona kuna sababu ya kukuunga mkono?

Muna: Hakuna ila kuna msanii kama Mboto, aliguswa na tatizo la mmoja wa watoto, akatoa kile alichojaaliwa.

UWAZI: Ni changamoto gani unakumbana nazo katika juhudi zako hizi?

Muna: Kama unavyojua, changamoto haziwezi kukosekana ila kikubwa nashukuru Mungu ananisimamia kwa kila jambo.

UWAZI: Hili la kusaidia watoto unalifanya chini ya taasisi flani au wewe tu?

Muna: Nina mpango wa kuanzisha kitu hicho, naamini nitatimiza hilo.

UWAZI: Wewe umeguswa na watoto hawa wanaoteseka, hujawahi kuzungumza na baadhi ya mastaa wenzako mkaona jinsi la kulifanya hili kwa nguvu ya pamoja?

Muna: Unajua kila mtu ana kitu chake anachopenda kukifanya katika jamii yake, huwezi kumlazimisha mtu afanye unachokifanya wewe.

UWAZI: Licha ya yote haya unayofanya, wapo watu ambao ‘wanakurushia mawe’ kwa kukusema vibaya, wewe unalichukulije hilo?

Muna: Siku zote ili dhahabu iwe nzuri lazima ipite kwenye moto kwanza ndio iwe dhahabu, hivyo maneno yananipa nguvu sana ya kusonga mbele.

UWAZI: Nakushukuru na nakutakia kila la heri katika jambo jema hili unalolifanya kwa nchi yako.

Muna: Asante sana.

Comments are closed.