The House of Favourite Newspapers

MUNA AOTESHWA NDOA MWAKA HUU

MUIGIZAJI wa filamu, Rose Alphonce ‘Muna’ amesema ameoteshwa na anaamini kabisa mwaka huu Mungu, atamletea mumewe kwa sababu hajawahi kumuomba kitu akaacha kumjibu kwa wakati hivyo ataolewa kabla mwaka huu haujaisha.

 

Akizungumza na Za Motomoto, Muna alisema kuwa siku zote katika maombi yake anamuomba sana Mungu, ampatie mume anayefanana na yeye kwa kila kitu na awe msaidizi wake wa maisha kitu ambacho anaamini maombi yake hayo yatapokelewa na mwaka huu jambo hilo litatendeka.

 

“Mungu wangu ninayemuamini hajawahi kuniacha hata siku moja na pia atanifanyia hili litendeke bila kipingamizi kwa sababu nimemuomba mume mwema na ninajua atanipatia kabla mwaka huu haujaisha kabisa na kila mmoja atashuhudia hilo,” alisema Muna.

Stori: Andrew Carlos

Comments are closed.