MUNA: MANENO YANGENIWEKA MBALI NA WOKOVU

Rose Alphonce ‘Muna’

MSANII wa filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’ amesema kuwa kama angesikiliza kejeli za watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii hakika as­ingekuwa na wokovu alionao mpaka Leo.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Muna alisema kuwa maneno ya kwenye mitandao yanaumiza sana kiasi kwamba kama mtu huna Mun­gu wa kweli huwezi kuvumilia na unaweza kujikuta unaweka wokovu pembeni.

“Kama nisingem­pokea Yesu vizuri maneno ya kwenye mitandao yangeniten­ganisha na wokovu kwani safari yangu ya kuokoka ingeishia njiani, Mungu alinisima­mia mpaka leo sijate­tereka,” alisema Muna.

Toa comment