Muna: Nikiwa Muislam Au Mkristo Haiwahusu

MUIGIZAJI wa filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’ amewacharukia wanaomsakama kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na dini ambayo mpaka sasa haieleweki ni Muislam au Mkristo kutokana na madai ya kufunga ndoa ya Kiislam wakati yeye ameokoka na kusema kuwa haiwahusu.

 

Akistorisha na Amani, Muna alisema kuwa yeye kuwa Mkristo au Muislam haiwahusu licha ya kwamba anaumia sana akiona anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii na wengine wakimponda kuhusiana na ulokole wake wakati hawajui nini kinaendelea kwenye maisha yake ya kila siku.

 

“Unajua watu wanapenda kumuona mtu akisononeka kila wakati au amebeba maumivu makali kwenye moyo ndiyo furaha yao, lakini mimi siwafuatilii acha waongee mpaka wachoke, sina muda ninajua nini ninachokifanya kwenye maisha yangu,” alisema Muna.

STORI NA IMELDA MTEMA | AMANI

Toa comment