The House of Favourite Newspapers

Muna: Sina kinyongo na Wema

0

MSANII wa filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna Love’ amesema kuwa hajawahi kuacha kumpenda msanii mwenzake Wema Sepetu licha ya mambo yote yaliyowahi kutokea kati yao.  Akizungumza na Risasi Vibes hivi karibuni ikiwa ni baada ya wawili hao kuonekana wameshamaliza tofauti zao, mwanamama huyo alisema kuwa, Wema ni mtu safi sana na mara nyingi sio mtu wa kukaa na kinyongo moyoni, ndio maana aliyapuuzia mambo yote na kuamua kurudisha urafiki wao ulioyumba hapo kati.

“Unajua mimi nampenda sana Wema na hata yeye mwenyewe analijua hilo na siku zote nimekuwa nikimuombea ili mambo yake yafanikiwe licha ya matatizo makubwa yaliyowahi kutokea baina yetu, hivyo kwa sasa tuko poa kabisa na hakuna shida yoyote kati yetu,” alisema.

Wawili hao walikuwa mashoga sana zamani lakini baadaye waligeuka maadui na kila mtu kumuona mwenzake mbaya, Wema alimmaindi vibaya Muna alivyojitapa kuwa ndiye anayemtafutia mabwana.

 

 STORI: Memorise Richard, Risasi

Leave A Reply