Muna: Tatuu na Ulokole Wangu Havihusiani

MSANII wa filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’ amefunguka kuwa, watu wengi wanamsema vibaya kutokana na ‘tatuu’ zake alizozichora mwilini kuwa haziendani na ulokole, jambo ambalo linamshangaza sana.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi Muna alisema, siku zote mtu anapoamua kurudi kwa muumba wake haangalii makosa ambayo ameyatenda nyuma, anachofanya ni kumpokea na kumsamehe kila kitu.

 

“Sidhani kama Mungu ataangalia tatuu zangu, ninachojua hatahesabu madhambi yangu bali atanipokea na kufuta kila kitu changu cha nyuma, sababu kama ni tatuu nilishazichora haina njia ya kuzikwepa na kwa sababu nimetubu naamini Mungu atanisikiliza,” alisema Muna.

STORI: IMELDA MTEMA

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment