The House of Favourite Newspapers

Klabu Billicanas Inavyozidi Kutoweka Ikibomolewa

1Eneo ambalo lilikuwepo klabu maarufu ya Billicanas ambalo linaendelea kubomolewa kutokana na kudaiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

DAR ES SALAAM: JENGO ambalo zamani lilijumuisha klabu maarufu ya Billicanas jijini Dar es Salaam iliyokuwa inamilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hivi sasa inaendelea kuwa stori ya zamani kwani litatoweka hivi karibuni kutokana na ubomoaji wa jengo hilo ambalo unaizi kushika kasi kila kukicha. Baada ya muda  sehemu hiyo itakuwa tupu kutokana na uvunjaji huo unaoendelea kutukoana na madai ya malimbikizo ya  deni lililofikia Shilingi bilioni 1.171.

 

3

Ubomoaji wa jengo la klabu ya Billicanas ukiendelea

Jengo hilo ambalo lilikuwa mali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  lilikuwa katika makutano ya Barabara ya Mkwepu na Indira Gandhi kitalu Namba 725-726/24 na hati Namba C.T. 186018 na CT 186018/10.

Mwanzoni mwa Septemba mwaka jana NHC ikishirikiana na kampuni ya Poster and General Traders, ilifika katika jengo hilo kwa maelekezo ya kutoa  samani mbalimbali zilizokuwa ndani yake na kumpa mmiliki (Mbowe) siku 14  kulipa deni ili kugomboa mali hizo.

4

Ubomoaji wa jengo la klabu ya Billicanas ukiendelea

Limbikizo hilo liliifanya NHC kuziondoa katika jengo hilo ofisi za magazeti yanayomilikiwa na  Free Media likiwemo Tanzania Daima kabla ya kubomoa  jengo hilo.

Comments are closed.