The House of Favourite Newspapers

Muonekano Mpya wa Ijumaa Wavutia Mbezi-Inn

0

1        Vasco Dau (kulia) na Sijali Khamis (katikati) wakifafanuliwa jambo na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.

2Mdau mkubwa wa Gazeti la Championi, Yusuph Athumani,  aliyekutwa akilisoma gazeti hilo pendwa na Ijumaa katika eneo la Kibamba.

3Victor January (katikati mwenye gazeti) akilisoma gazeti la Ijumaa sambamba na wasomaji wengine waliokuwa wakifuatilia kilichoandikwa ndani yake.

4 Msomaji wa Ijumaa aliyejitambulisha kwa jina la Jasu Perpect (kushoto) akiwa na rafiki yake wakisoma gazeti la Ijumaa.

5Wasomaji wa Ijumaa wakipozi na muuzaji wa magazeti ya Global, Mwamvita Rashid (wa pili kulia) katika eneo la Mbezi-Inn.

6Monica Tahani akifafanuliwa jambo na Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub.

7Mwanadada aitwaye, Zay, anayefanya shughuli zake katika saluni yake iitwayo ‘Zay Salon’ katika eneo la Mbezi-Inn akimwonesha ukurasa wenye hadithi mteja wake. Anayewashuhudia kulia ni Ofisa Usambazaji, Jimmy Haroub.

8Msomaji wa Ijumaa, Clement Mlay, akilisoma gazeti hilo.

9Oswald Philemon (wa pili kushoto) akiwa na mafundi gereji wenzake katika kulisoma gazeti la Ijumaa.

 

GAZETI la Ijumaa lenye muonekano mpya leo Ijumaa lilikuwa kivutio kikubwa baada ya wasomaji wake wa Mbezi-Inn jijini Dar es Salaam kulinunua kwa wingi wakisema wanalikubali kwa habari zake za burudani na michezo.

Timu ya gazeti hilo imetinga eneo hilo na kuzunguka sehemu mbalimbali ambapo wadau kibao walionekana wakiwa wamelinunua na wakaeleza wanakubali mabadiliko yaliyofanyika.

Walisema  kinachowavutia zaidi ni habari na makala mbalimbali zinazowahusu mastaa ambazo zinawafanya wasuuzike roho zao wanapolisoma.

“Ijumaa ndiyo gazeti bora Bongo, habari zake na makala ni burudani tosha hasa ukichukulia kwamba ndilo linaloandika habari za mastaa kwa undani,” alisema Monica Tahani mkazi wa Mbezi.

Akizungumza na wakazi eneo hilo, Yohana Mkanda ambaye ni Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers Ltd inayozalisha gazeti hilo pamoja na Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, na Championi, aliwaomba wasomaji wa magazeti hayo kuendelea kulinunua Ijumaa kwa bei ya Sh.1,000 kwani thamani ya kilichomo ndani yake ni zaidi ya bei hiyo.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply