The House of Favourite Newspapers
gunners X

Muroto: Atakayeandamana Dodoma Kesho, Atapigwa, Atachakaa – Video

BAADA ya vijana wa chama cha ACT-Wazalendo kutangaza maandamano kesho Aprili 9, 2019 kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi jijini Dodoma kushinikiza Bunge la Tanzania kufuta azimio lake la kutofanya kazi na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto ametoa onyo kwa watu waliopanga kufanya maandamano hayo wasifanye hivyo.

 

Amesema hayo leo Aprili 8, 2019 wakati akizungumza na wanahabari jijini humo kuwa taarifa wamezipata kupitia mitandao ya kijamii hivyo jeshi lao limejipanga na linawasubiri waandamanaji hao waingie barabarani hapo kesho, wakione cha moto.

 

“Tunazo taarifa zinazotembea mitandaoni kwamba chama cha ACT-Wazalendo, kushirikiana na Chauma, UDP na vyama vingine, wamepanga kufanya maandamano kesho, hivy0 nataka kuwaambia hao wanaohamasisha maandamano kuwa, wakiingia tu barabarani kama wanavyohamasisha, watapigwa, watachakaa, narudia tena, watapigwa, watachakaa.

 

“Sisi tupo tayari, tunafanya mazoezi muda wote, hivyo tunawasubiri. Maandamano hayo si halali.  shughuli za Bunge zinaendelea kama kawaida, wananchi waendele na shughuli zao kwani sisi tupo kwa ajili yao kuhakikisha usalama upo Dodoma,” amesema Muroto.

MSIKIE MUROTO AKITOA ONYO

Comments are closed.