The House of Favourite Newspapers

Museveni Aapishwa Kuwa Rais wa Uganda

0

Rais Yoweri Musevei baada ya kuapishwa.

Yoweri Museveni leo ametawazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Uganda kwa muhula wa tano mfululizo.Tayari Rais Museveni amekwisha tawala miaka 30. Kutawazwa kwake leo, ambako kunashuhudiwa na viongozi wa mataifa 14 kutoka Afrika na wageni wengine mashuhuri, kuna fuata ushindi uliojaa ubishani katika uchaguzi wa Februari 18.

14.18pm:Katika ufisadi Museveni amesema kuwa kucheleweshwa kuchukuliwa kwa hatua kunawaudhi raia na kutowavutia wawekezaji

14.16pm:Amesema kuwa Uganda imekuwa na amani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 500.”Hakuna mtu anayeweza kuharibu usalama wa Uganda”.Amewataka wenzake wa Afrika kuimarisha usalama wa Somalia na Congo

14.11pm:Amewataka wakulima kulima kahawa na chai.Amesema kila nyumba lazima ishiriki katika kilimo.

13.57pm:Museveni amesema kuwa Uchumi wa Uganda umekuwa sana lakini tatizo ni kwamba Waganda wamekuwa wakinunua vitu vingi kutoka nje na kuuza nje vichache.

 

Amewapongeza raia wa Uganda kwa kupiga kura kwa wingi katika kila sekta ya uongozi.Vilevile amevipongeza vyama vya upinzani kwa kushinda viti mbali mbali.

13.45pm:Rais wa Chad Idris Deby amehutubia kwa lugha ya kifaransa.

13.33pm:Museveni asema ICC ni bodi isiyo na maana.”Tuliunga mkono icc tukidhani ni mahakama nzuri lakini baadaye tukagundua ni mahakama yenye watu wasio na maana”.Museveni ameyasema hayo baada ya kumtambua rais wa Sudan Omar el Bashir

13.23pm:Baadhi ya viongozi waliotambuliwa katika sherhe hiyo ni rais Uhuru Kenyatta wa kenya

Yoweri museveni amkaribisha rais wa Zimbabwe,Omar el bashir wa Sudan.

Rais wa Sudan Omar el Bashir

13.17pm:Miongoni mwa marais wanaohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na rais wa Sudan Omar el Bashir anayeswaka na mahakama ya uhailifu wa kivita ICC kwa madai ya kutekeleza uhalifu katika eneo la Darfur na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

13.13pm:Jeshi la Uganda latoa heshima zao kwa rais Museveni hivi sasa.

13.09pm:Wimbo wa taifa unaimbwa

12.56pm:Ni wakati ambapo ndege za jeshi zinatoa heshima zao kwa rais Museveni.Ndege hizo zinaonyesha uwezo wake wa kulilinda taifa la Uganda chini ya uongozi wa rais Museveni.

12.38pm:Museveni amekabidhiwa vifaa muhimu vya madaraka ikiwemo katiba,ngao ya mamlaka,bendera na upanga ambao ni ishara ya jeshi.

Na sasa ni zamu ya jeshi la taifa hilo kumpatia heshima rais huyo.

Jeshi la Uganda

12.15pm:Rais Museveni alikagua gwaride la jeshi baada ya kuapishwa rasmi

12.10pm:Rais Yoweri Museveni aapishwa rasmi na jaji mkuu

Baadhi ya watumbuizaji wa hafla hiyo

12.05pm:leo rasmi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko ili watu watokeze kwa wingi kwa sherehe hizo. Ingawaje bado kuna hali ya wasiwasi kwa vile chama cha upinzani na FDC na mgombea urais wa zamani Dk Kizza Besigye bado wanakana ushindi wa Museveni.

12.00pm:Rais Yoweri Museveni kuapishwa kuwa rais kwa muhula wa saba mfululizo nchini Uganda

Museveni kumkabidhi madaraka Museveni si jipya kwa Waganda. nani Rais ambaye alilaumu mwaka 1986, viongozi wa Afrika kukaa madarakani kwa muda mrefu sana.

Leave A Reply