The House of Favourite Newspapers

Museveni Awataka DRC Na M23 Wakutane

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesisitiza umuhimu wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) kufanya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja na kikundi cha Waasi wa M23 ili kukomesha vita inayopiganwa mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Museveni amesema vita hivyo haviwaathiri DRC na M23 pekee bali nchi yake Uganda na eneo zima la kanda ya Afrika Mashariki.

Katika hatua nyingine Rais Museveni amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na mkutano wa pamoja kati ya Nchi wanachama wa SADC na EAC ili kuruhusu Rwanda na Congo zote kukutanishwa pamoja katika kujadili namna bora ya kumaliza vita hiyo.