The House of Favourite Newspapers

Museveni Azindua Basi la Kutumia Nishati ya Jua

0

MUSEVEN (2) Basi linalotumia nishati ya jua lazinduliwa nchini UgandaMUSEVEN (3) Museveni akizindua basi la kutumia nishati ya jua nchini UgandaMUSEVEN (4)

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezindua basi la kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki linalotumia nishati ya jua.

Mabasi hayo yalitengezwa nchini Uganda na kampuni ya magari ya Kiira Motors Kayoola.

Moja ya betri zake inaweza kutiwa chaji na vibamba vyenye chaji ya mionzi ya jua vilivyopo katika paa la magari hayo ambavyo huongeza kasi ya gari hilo kufikia kilomita 80.

Basi hilo lenye viti 35 linatarajiwa kutumika mijini badala ya miji mikuu kutokana na masharti ya umbali wa usafiri wake.

Iwapo yatatengezwa kwa wingi, kila basi linaweza kugharimu dola 58,000 ambayo Bw. Musaizi anasema ni bei nzuri katika soko.

Kampuni ya magari ya Kiira Motors ilikuwa kufuatia mradi wake katika Chuo Kikuu cha Makerere, nchini humo ambacho kinamiliki hisa katika kampuni hiyo na ambacho pia kimefaidika na fedha za serikali.

Leave A Reply