The House of Favourite Newspapers

Museveni, Kagame Wamaliza Tofauti Zao

MARAIS Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda, kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.

Walifikia makubaliano hayo katika mkutano huo wa pili mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Angola na  Congo Brazzaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

 

Joto la kisiasa limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.

Maofisa nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

 

“Tutashughulikia matatizo haya yote,”  Rais Kagame amewaambia waandishi habari baada ya kusaini makubaliano hayo.

 

 

Viongozi hao wawili wamekubaliana kutilia mkazo kutatua mzozo wowote baina ya mataifa yao kwa njia amani, shirika la habari nchini Angola, Angop, linaripoti.

Comments are closed.