The House of Favourite Newspapers
gunners X

Musukuma Adai RC Gabriel na Wenzake Wametafuna Mil 600 – Video

0

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma amemlipua mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel na timu akidai wamepata zaidi ya Sh600 milioni kutoka katika fungu la fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zinazotolewa na mgodi wa dhahabu wa Geita.

 

Musukuma ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 29, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2021/22.

 

Amesema halmashauri ya Wilaya ya Geita inapata fedha za CSR kiasi cha Sh10 bilioni kwa mwaka lakini hazina mpangilio.

 

“Ni kama kitu kimetupwa hakina mwenyewe. Ni kwa nini nyinyi Wizara ya Madini na Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) mkampa mamlaka mkuu wa Mkoa ya kuamua fedha za halmashauri?”

 

“Ajenge darasa, ajenge hoteli kuna vitu vingine vinauma, ninazo nyaraka hapa kwa mwaka Geita na Geita Mjini, mkuu wa mkoa na timu yake wamejilipa posho ya Sh600 milioni kitu ambacho hakiwezekani” amesema.

Leave A Reply