MUTRAH ‘AWALILIA’ WANAOTOA MIMBA

Mutrah Tamim

MUIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Mutrah Tamim ‘amewalilia’ wasichana wanaotoa mimba kila kukicha na kuwataka waache kwani watoto hao watakuja kuwa msaada kwao hapo baadaye. 

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Mutrah alisema hakuna raha kama kuwa na mtoto hivyo kuwaomba wasichana wanaopenda kutoa mimba pindi wanapozipata waache mara moja na kama wanajiona hawapo tayari kuzaa basi wasishiriki kabisa tendo la ndoa mpaka pale watakapokuwa tayari kuzaa

“Unajua hakuna kitu kizuri kama kuwa na mtoto maana ana raha yake sana katika familia yaani mimi tangu nimekuwa na mtoto najikuta nina furaha tu muda wote hata nisipokuwa na hela najihisi kama ninayo vile, hivyo nawasihi hawa wasichana ambao wakipata mimba tu wanakimbilia kutoa waache kwa sababu watakuja kujutia wanachokifanya,” alisema Mutrah ambaye hivi karibuni alipata mtoto wa kike aitwaye Sherine

Toa comment