The House of Favourite Newspapers

Muuguzi Aliyepata Coronavirus Ajiua

0

MUUGUZI aliyekuwa akifanya kazi katika Kitengo Maalum cha Kupambana na Maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Italy, Daniela Trezzi (34) amejiua kutokana na hofu ya kusambaza #COVID_19 kwa wengine.

 

Gazeti la Daily Mail limesema muuguzi huyo aliyekuwa akifanya kazi katika Hospitali ya San Gerardo, alikuwa na msongo wa mawazo wakati akihudumia watu waliokumbwa na ugonjwa huo na hali yak ilizidi kuwa mbaya alipogundulikakuwa na Covid-19 siku ya Machi 10, 2020.

 

Muuguzi huyo anadaiwa kuwaambia watu aliokuwa akifanya nao kazi kwamba alikuwa na wasiwasi  huenda alikuwa amewaambukiza  watu wengine virusi hivyo.

 

Meneja wa hospitali hiyo, Mario Alparone, alisema Trezzi alikuwa nyumbani akijiuguza na “hakuwa chini ya ulinzi.”

 

Source: Hollywoodunlocked.com

Leave A Reply