The House of Favourite Newspapers

Muuza Bangi Aingia Kimakosa Ndani ya Gari la Polisi Akidhani ni Teksi

MTU mmoja anayedaiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya amejikuta akipata wakati mgumu katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismasi baada ya kuingia kwenye teksi akiwa na misokoto takribani 1000 ya bangi pasipo kufahamu kuwa anaingia kwenye gari la polisi.

Tukio hilo la aina yake limetokea hivi karibuni katika eneo la Christiana, Mji Mkuu wa Copenhagen maarufu kwa biashara ya madawa ya kulevya nchini Denmark ambapo inasemekana mwanamume huyo alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwenye biashara zake hizo haramu.

Polisi wameeleza kufurahishwa na ufanisi wa tukio hilo kwani mtuhumiwa huyo walikuwa wakimsaka muda mrefu hivyo wamemfunguliwa mashtaka ya kuhusika na biashsra ya madawa ya kulevya.

Nchini Denmark, biashara ya madawa ya kulevya ni haramu na Wilaya ya Christiana miezi ya hivi karibuni msako mkali ulifanyika kuwatafuta wauza madawa ya kulevya .

Comments are closed.