The House of Favourite Newspapers

Muuza Matunda Wa Chamazi Ajishindia Mil 100 za Gal’s Sports Betting

Kampuni ya Gal Sports Betting inayojighulisha na ubashiri wa matokeo ya mechi mbalimbali imemkabidhi hundi ya Mil.100 mshindi aliyeibuka na zawadi nono ya kitita hicho cha Shilingi za Kitanzania Milioni Mia Moja(100,000,000), Juma Yusuph Kidoga mkazi wa Chamazi Dar.

Juma amefafanua kuwa shughuli anayojishughulisha katika maeneo yake ni kuuza matunda. Akikabidhiwa hundi yake Juma ameeleza kuwa ‘ Amekua akibashiri matokeo ya mechi na kampuni ya Gal Sports Betting kwa takribani miezi mitatu sasa, kwa kupenda kwake mchezo wa mpira wa miguu amejikuta anaingia katika mchezo huu wa ubashiri wa matokeo ya mechi jambo lililopelekea kuibuka mshindi wa kitita hicho cha fedha (milioni mia moja’.

“Nina furaha kubwa kuwa mshindi wa kiwango kikubwa cha fedha kama hiko. Nitazitumia fedha hizo kuwasaidia wazazi wangu walioko Tanga ili nipate baraka zao kwanza kabla ya kuanza kutafakari ni kwa namna gani nitazitumia fedha zangu za ushindi” Alisema Juma.


“Kwa muda mrefu nilipoteza ndoto yangu ya kujishughulisha na uuzaji wa vifaa vya umeme, jambo ambalo nitalifanikisha kwa kutumia fedha hizi. Najiona muuzaji mkubwa wa vifaa vya umeme hapo baadae” Aliongeza Juma.
“Tulianza kufanya shughuli zetu Tanzania tangu mwaka 2016. Kampuni yetu inaongoza kwa kuwa na maduka mengi na yenye ubora wa huduma kwa wateja wetu. Viwango vyetu vya ubashiri ni ya hali ya juu nchi nzima” Alieleza Mkurugenzi wa Gal’s Sports Betting Bw. Hakan Aric.

“Tutaongeza bidhaa zaidi kwenye wasifu wetu ili kuongeza burudani jambo litakalo panua wigo wa ushindi kwa wateja wetu. Bila shaka tunajinadi kuwa miongoni mwa wachache wanaotoa zawadi stahiki kwa washindi bila kuchelewa” Aliongeza Bw. Aric Kuhusiana na Gal’s Sports Betting Juma anashauri kutokata tamaa na daima kuwa na imani juu ya matokeo chanya wakati wa kufanya ubashiri, kwa Juma ubashiri ni nafasi ya kupumzika kwani inamlazimu kuwa makini wakati wa kufanya ubashiri.

Comments are closed.