The House of Favourite Newspapers

Muuza Mitumba Ashinda 500,000 Chemsha Bongo Na Amani

1116f3b4-2521-4f92-a3f4-fa51b25a0051

Mfanyabiashara wa Mitumba, Sikitu Piallo akiwa katika pozi.

MWANAMAMA, Sikitu Piallo (29) Mkazi wa Kantalamba-Sumbawanga mkoani Rukwa ambaye ni muuza mitumba, ameshinda shilingi 500,000 katika chemsha bongo ya kwenda Dubai inayotolewa na Gazeti la Amani.

Akizungumza na mtandao huu  mara baada ya kupigiwa simu kama mshindi, Sikitu ambaye ni mama wa mtoto mmoja mwenye miaka miwili alisema, zawadi tangu ameanza kushiriki chemsha bongo mbalimbali hii ni kubwa na ya kwanza kwake.

“Kwa kweli sijui hata nisemaje! Nimefurahi sana Mungu awabariki, ni vigumu kuamini lakini nimeshinda kweli jamani uuhhh!,” alisema Sikitu.

Sikitu aliongeza kuwa, zawadi hiyo imekuja muda muafaka katika kipindi hiki kwani kitarahisisha maisha yake.

“Ujue mimi ni mfanyabiashara, kazi yangu nauza mitumba. Siku nyingi nimekuwa nikihangaika na mtaji mdogo lakini sasa Mungu ameweza kufungua milango na sasa nitaongeza mtaji, asanteni sana!” Sikitu aliendelea kushukuru.

Akizungumzia chemsha bongo inayotoka katika gazeti hilo, Sikitu alisema kuwa, amekuwa msomaji wa magazeti pendwa kwa muda mrefu.

“Hakuna kitu ninachokipenda katika magazeti pendwa kama katuni na vichekesho, napenda kwa sababu mara nyingi inaniongezea siku za kuishi, haa haa haa!” alimaliza Sikitu kwa kucheka.

Chemsha bongo hii ni ya nne tangu kuanza, hadi sasa washiriki wote wameshajilambia shilingi 500,000 ambazo zimerahisisha maisha yao. Washindi waliopita ni Jimmy Kisanga kutoka Mwanza, Godwin Deodath Katiali mkazi wa Njia Panda Machame, Moshi pamoja na Bakari Omar Omunga mkazi wa Manzese jijini Dar.

Chemsha Bongo hii bado inaendelea katika gazeti lako la Amani. Ili kushiriki ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kununua gazeti lako hilo kila Alhamisi na kujibu swali kiufasaha linalopatikana ukurasa wa pili. Kumbuka mshindi pia anaweza kupata safari ya kwenda kwenye jiji la maraha duniani, Dubai kula bata kwa siku tatu.

Comments are closed.