The House of Favourite Newspapers

MUVI YA CHEMICAL, WEMA YAZUA JAMBO

Image result for Claudia Lubao ‘Chemical’,
Claudia Lubao ‘Chemical’

HIVI karibuni rapa wa kike kunako Muziki wa Bongo Fleva, Claudia Lubao ‘Chemical’, aliweka kwenye Mtandao wa YouTube, vipande vya filamu yake iitwayo Mary Mary, ambayo ameigiza akiwa na mrembo, Wema Sepetu na kuzua jambo baada ya mashabiki wengi kutoridhishwa nayo.

Baada ya kuweka vipande vinne, mashabiki waliibuka na kuanza kuichambua muvi hiyo ambapo mbali na pongezi za stori kuwa nzuri, walimchana kwamba amerudia makosa mengi ambayo muvi nyingi za Kibongo zinayo. Mfano wa baadhi ya makosa hayo ambayo mashabiki waliyachambua na kudai ni ya kitoto na yanakera, ulikuwa ni uhusika wa Wema kwenye filamu hiyo. Wema aliigiza kama mwanadada wa kijijini ambaye anaishi kwenye maisha magumu na anapambana na hali yake kila siku kwa kutafuta kipato chake akiuza mihogo.

Lakini akiwa katika hali hiyo, Wema anaonekana akiwa na ‘tatuu’ za maana, amependeza kimuonekano na haakisi hata kidogo muonekano kama alikuwa ni msichana wa kijijini, lakini kilichoshangaza zaidi alikuwa anamfokea Chemical, kuhusu aina ya unyoaji wake kwamba unakiuka maadili wakati yeye mwenyewe akiwa amechora tatuu kila kona.Related image

Kosa lingine ambalo lilionekana ni la kitoto ni pale ambapo mtu anaonekana anatembea takribani dakika moja huku hakuna ambacho anakifanya. Lakini pia dosari nyingi zimechambuliwa kwenye kuediti na mambo mengine.

Hivyo ni vipande vinne tu ambavyo vimewekwa, pengine dosari nyingine zitaonekana mbeleni.Kwa upande wa Chemical alipotafutwa kuzungumzia juu ya makosa hayo alisema; “Hakuna kizuri ambacho hakiwezi kutolewa kasoro. Kikubwa tu Watanzania watupe sapoti kwenye kazi yetu hii kwa sababu ni mwanzo, panapoonekana kuna makosa ni msaada wetu baadaye.”

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.