The House of Favourite Newspapers

Mv.Sabasaba Yakabidhiwa Kuanza Safari Kisiwa cha Kome-Nyakariro Buchosa

0

 

Wananchi wa Kome- Buchosa wameondokana na adha ya usafiri baada ya kupata usafiri mpya wa kivuko cha Mv. Sabasaba

WANANCHI wa kisiwa cha Kome Halmashauri ya Buchosa wilayani  Sengerema Mkoa wa Mwanza wameondokana na adha ya usafiri baada ya Serikali kukabidhi kivuko cha Mv.Sabasaba kitakachotoa huduma ya usafiri kwenye kisiwa hicho kikisaidiana na kivuko cha Mv.Kome II kinachotoa huduma kwa sasa.

 

 

Meneja wa wakala wa ufundi Mkoa wa Mwanza (Tamesa)  Aloyce Ndunguru amesema kivuko cha mv.Sabasaba kimekarabatiwa kwa Sh239milioni ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma ya usafiri kwenye kisiwa cha kome.

 

Amesema kivuko hicho kina tani 85 uwezo wa kubeba abiria 330 na magiri kumi madogo madogo huku kivuko cha Mv.Kome II kina tani 40 uwezo wa kubeba abiria 120 na magari 5 hivyo ujio wa kivuko cha mv Sabasaba kitakuwa mkombozi kwa wakazi wa kisiwa hicho.

 

Licha ya kukabidhiwa  kivuko hicho pia amesema Serikali imeandaa kivuko kingine Kipya kitakacho gharamu Sh8 bilioni ambacho kitakuwa na uwezo wa kubeba magari 22 na abiria 800 ,abiria 400 wakiwa wamekaa na abiria 400 wakiwa wamesimama ambapo kikikamilika kitatoa huduma kwenye kisiwa Cha Kome.

 

“Kivuko hiki nichamuda wakati kivuko kipya kinatengenezwa   kitakapokamili kitakuja kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa Kome na adha ya usafiri kwenye kisiwa cha Kome itakuwa imemalizika,amesema Ndunguru.

 

Baadhi ya wananchi wa kisiwa cha Kome Arodia John wamefurahishwa na kitendo cha serikali kuleta kivuko cha mv Sabasaba ambacho kitawasaidia wananchi wa Kome kuondokana na adha ya usafiri.

 

Amesema kivuko cha Mv Kome II kilikuwa  kimelemewa na abiria hivyo uwepo wa kivuko cha Mv Sabasaba kimeondoa adha hiyo.

Kivuko cha Mv. Sabasaba

Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amesema moja ya ahadi yake ilikuwa nikuleta kivuko kipya kwenye kisiwa cha Kome na kuwaondolea adha wakazi wa Kome.

 

“Kipindi cha kampeni mwaka 2020 niliwaambia wakazi wa kisiwa cha Kome kuwa kama sitaleta kivuko kipya wasinichangue tena hivyo ahadi nimetimiza na kivuko kimepatikana na wananchi wanafurahia,amesema Shigongo.

 

Asilimia 90 ya wakazi wa kisiwa cha kome wanafanya shughuli za Uvuvi ,kilimo na ufugaji hivyo ujio wa kivuko hiki kitawasaidia kufanya biashara zao.

 

Mwenyeki wa CCM wilaya ya Sengerema Marco Makoye amesema Ilani ya CCM jimbo la Buchosa inatekelezwa kwa vitendo na chama cha mapinduzi hakina shaka na jinsi Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo anavyotekeleza ilani ya CCM kwa vitendo.

 

 

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga ambaye alikuwa mgeni rasimi kwenye hafla ya kukabidhi kivuko hicho amewakata wananchi kukitunza kivuko hicho ili kiwasaidie.

 

Ameserikali Serikali inatafuta fedha huku na kule ili kuwaletea wananchi maendeleo hivyo kupatikana kwa kivuko hiki ni neema ambayo wananchi wameipata.

 

Kivuko cha Mv Sabasaba kimekabidhiwa kwa wananchi wa kisiwa cha kome ambao walikuwa wanakumbana na adha ya usafiri kutokana na kivuko cha Mv Kome II kuelemewa na abiria.

Leave A Reply