MVP wa Ligi Kuu Aziz Ki Aeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni Kubeba mataji
MVP wa Ligi Kuu Bara 2023/24, Aziz Ki ameweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kuona wanatwaa mataji ili kuendeleza furaha ndani ya timu hiyo.
Ki anaingia kwenye orodha ya mastaa waliotwaa tuzo zaidi ya moja kwenye usiku wa tuzo zilizotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).
Ni MVP, kiungo bora, mfungaji bora alifunga mabao 21 na pasi 8 za mabao na jina lake lipo kwenye orodha ya kikosi bora msimu wa 2023/24.
Ki bado yupo ndani ya Yanga baada ya kuongeza kandarasi mpya kuendelea kutimiza majukumu yake ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Miguel.
Kiungo huyo amesema: “Furaha kubwa ni kuona timu inatwaa ubingwa suala la tuzo sio kipaumbele kikubwa lakini linapotokea inakuwa ni furaha kwangu na timu kiujumla.
“Ushirikiano kutoka kwa wachezaji ni jambo kubwa na msingi hivyo tuendelee kuwa pamoja kwenye msimu mpya.”