The House of Favourite Newspapers

Mvua Ilivyosababisha Maafa Dar

MVUA za masika zinazoendelea kunyesha zilisababisha maafa makubwa ikiwemo vifo vya watu wanne pamoja na watu kadhaa kujeruhiwa na ukuta wa kiwanda cha Pepsi kilichopo Barabara ya Nyerere jijini Dar kuanguka.

 

Waandishi wetu walizunguuka viunga mbalimbali vya Jiji la Dar na kujionea barabara nyingi maeneo ya Tabata, Kigogo, Yombo, Msasani, Mikocheni, Kawe, Kimara, Tandale zikishindwa kupitika kufuatia madaraja na makaravati kuzolewa na maji huku nyingine zikiwa zimechimbika na madimbwi kujaa maji.

Kama kawaida Bonde la Jangwani hali ilikuwa mbaya zaidi hali iliyosababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya Magomeni Mapipa na Faya hivyo mabasi ya mwendo wa haraka na vyombo vingine vya usafiri kushindwa kutumia njia hiyo.

 

Akizungumza, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,(SACP) Lazaro Mambosasa alisema mpaka kufikia jana Jumatatu, alishapokea taarifa ya vifo vya watu tisa huku mmoja mwili wke ulipatikana akisombwa na mafuriko kuelekea Jangwani.

Akifafanua tukio hilo, Kamanda Mambosasa alisema maiti ya kijana mmoja anayekadiliwa kuwa na umri miaka 20 mpaka 25 imekutwa ikielea kwenye bonde la Tabata Kisiwani.

 

Alisema sambamba na tukio hilo nyumba moja iliyoko hukohuko Tabata ukuta wake umeanguka na kusababisha kifo cha mama na mwanaye.

Sambamba na vifo hivyo, Kamanda huyo amesema ukuta wa Kiwanda cha Pepsi kilichopo Barabara ya Nyerere umeangukia nyumba za majirani ambapo watu ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali.

 

Wakati akisema hayo ukuta wa moja nyingine iliyopo Kigogo Mbuyuni nao umeanguka na kusababisha kifo cha mwanamke mmoja ambapo mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kukuta mwili umeshaondolewa na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mwandishi wetu alimuulizia tukio hilo Kamanda Mambosasa ambapo alisema mpaka muda huo lilikuwa bado halijamfikia.

 

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Comments are closed.