The House of Favourite Newspapers

Mvua ya Upepo na Mawe Yaharibu Nyumba 479 na Kujeruhi 13

0

KWIMBA, MWANZA: Watu 13 wamejeruhiwa na takribani Nyumba 479 zimeharibiwa na mvua ya upepo na kusababisha watu 2,375 kukosa makazi.

Miongoni mwa majengo yaliyoharibika kutokana na mvua hiyo ni madarasa 2 ya Shule ya Msingi Mangulumwa na maabara ya Shule ya Sekondari Igongwa.

Akizungumza na Mwananchi baada ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mtemi Msafiri amesema kati ya majeruhi hao, mmoja ni Shida Masuka (10), mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mangulumwa.

Amesema mwanafunzi huyo amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Majeruhi wengine waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba wametajwa kuwa ni Shani Shija (11), Mashara Luhemea (11) na Angelina Pastori (11), wanafunzi wa Shule ya Msingi Mangulumwa na mkazi wa kijiji hicho, Mpemba Lufuga.

Leave A Reply