The House of Favourite Newspapers

Mwaka 2016, malkia/ mfalme wangu ni wewe

0

Maybe, will we stay all day in bed?

Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuuona Mwaka 2016, ikiwa ni siku ya nne tangu mwaka huu mpya uanze.

Wapo waliotamani kuuona lakini imeshindikana kwa mapenzi ya Mungu, wapo waliouona wakiwa na majanga tele, wengine wakiwa wamelazwa, wengine wakiwa ni walemavu kwa sababu mbalimbali.

Safu hii pendwa ya XXLove iko nawe bega kwa bega kwa shida na raha bila kujali kilichokufika, tunaamini sote tu waja wa Mungu.

Mada ya leo inazungumzia zaidi kuhusu wapenzi waliogombana, waliotengana, walioumizwa, kuachwa na kadhalika, kuuanza Mwaka 2016 kwa kufikia na kuwaza mazuri.

happy-couple-watching-tv-bedroomMsogelee mwenzio kwa karibu kama uko naye, mtumie SMS au mpigie simu na umwabie ‘mwaka 2016, malkia/mfalme wangu ni wewe’, inawezekana mliishi na mwenzako, yaani mchumba, mumeo, mkeo au wapenzi kwa bifu zito, kwa kununiana, kutukanana, kupigana, kusalitiana na mengineyo.

Sasa mwaka mpya umeanza, sema basi, nahitaji kutengeneza na kuanza uhusiano wagu upya. Ahidi familia, ndoa, uhusiano au mapenzi yako kuwa bora na ya kuigwa kwa Mwaka 2016. Achana na yote uliyotendewa na mpenzi wako, mumeo, mkeo, rafiki, ndugu na kadhalika, sasa songa mbele.

Naamini utakuwa unaukumbuka msemo huu; mwaka mpya na mambo mpya, basi msogelee mpenzi wako huko aliko na umwambie kuwa yeye ndiye malkia au mfalme wa moyo wako.

Mwambie mpenzi wako, mumy, baby nakupenda, napenda umbo lako, sura, rangi, nywele, macho, midomo na tabasamu lako.

Wewe ndiye faraja ya moyo wangu, wewe ndiye tiba ya maradhi yangu sugu yanayonisumbua, wewe ndiye mchumba, mpenzi, mke au mume bora.
Hakika kwangu wewe ni malkia, wewe ni mfalme katika ulimwengu wangu wa mahaba, kwako nimetulia.

Sina maua, sina kadi, sina fedha, nyumba wala gari, zaidi ya upendo na kukuthamini siku zote za maisha yangu.Wengi walisubiri tuachane tangu mwaka jana, kuna wakati tunakwazana, tunagombana na kadhalika lakini mwaka huu naomba tumalize tofauti zetu.

Pamoja na maumivu ya kuumizwa, basi nami najipa tumaini jipya la kumpata yule atakayenipenda kwa dhati mwenye penzi la kweli.Dunia ina watu na viatu, wapo waliosambaza umbeya kutugombanisha lakini wameshindwa, wewe ni yuleyule, michepuko tupa kule.

Tukutane wiki ijayo kwenye mada nyingine nzuri na tamu. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram kujua mengi kuhusu mapenzi.Ng'osha2

Leave A Reply