The House of Favourite Newspapers

Mwaka Wa 19 Anatembea Na Uvimbe Mkubwa, Unatoa Vidonda Na Uchafu – Video

Kalume Ally Kalume, mkazi wa Lindi.

Kama umezaliwa mzima na hujawahi kupata mitihani mikubwa ya maradhi katika maisha yako, unapaswa kumshukuru sana Mungu wako!

Kalume Ally Kalume, mkazi wa Lindi na yeye alitamani kuwa na furaha kama ilivyo kwa watu wengine, lakini kutokana na ugonjwa mbaya uliompata wa kuota nyama sehemu mbalimbali za mwili wake, ameteseka kwa takribani miaka 22 huku akishindwa kufanya chochote.

Akizungumza kwa uchungu na maumivu makali, Kalume alisema mpaka kufikia hapo alipo ni ukosefu wa fedha tu kwani angeshatibiwa na pengine angeshapona lakini hana fedha za kwenda hospitali na matokeo yake ni kwamba kila kukicha nyama zinazidi kuongezeka ukubwa kwenye mwili wake.

Kalume anawaomba Watanzania wamsaidie kwa hali na mali ili apate matibabu kwani hajui nini itakuwa hatima ya maisha yake.

“Silali mchana wala usiku, na nikilala kidogo usiku napata taabu maana lazima nikumbatia hili nyama kama mtoto, naombeni msaada jamani niende Muhimbili nikapate matibabu stahiki,” alisema Kalume.

Kama unataka kumsaidia chochote Kalume tuma kwenda namba 0655 104 668 (Salumu Hidobelele).