visa

MWAKIBINGA: WAPINZANI WANAHAMA KWA KUVUTIWA NA JPM

 

James Mwakibinga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo.

KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), James Mwakibinga amesema sababu zinazowafanya wanasiasa wa upinzani kuhamia CCM ni utendaji kazi wa Rais John Magufuli hasa katika kusimamia maendeleo ya nchi ikiwemo kupiga vita ufisadi.

 

Mwakibinga ameipongeza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuwa inafanya kazi nzuri kwani imefanya jambo la msingi kumshikilia Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Khamis kwa tuhuma za kutoa rushwa akiwa mkoani Dodoma, akisema kwa kipindi cha serikali ya awamu ya tano hakuna suala la kuendelea kuvumiliana katika kutenda maovu.

 

Aidha amempongeza mwenyekiti mpya wa UVCCM, Kheri James, kwa kuchaguliwa katika kakao cha wajumbe huko mkoani Dodoma.
Toa comment