Mwakinyo Apanda Viwango vya Dunia

Bondia wa Kimataifa kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo (26) mwenye uzani wa Super Welter amepanda kutoka nafasi ya 14 hadi nafasi ya 10 katika viwango vya ubora Duniani kwenye orodha ya mabondia wenye uzani huo.

Mwakinyo sasa amekuwa wa 10 kati ya mabondia 1,532 duniani ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kumtwanga Bondia wa Kimatifa kutoka nchini Namibia, Julius Munyelele Indongo.

Mwakinyo kwa sasa ana nyota 4, katika upande wa mabondia wa uzito wake na pambano lake la mwisho aliibuka na ushindi dhidi ya Julius Indongo kutoka Namibia.

Katika pambano hilo Mwakinyo alishinda kwa TKO raundi ya 4, pambano ambalo lilipigwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.

 2173
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment