Habari Mwakinyo Balaa! Atwaa Ubingwa Wa WBO Africa Middle Weight Kwa Kumzibua Mtu KO Last updated Jan 28, 2024 0 Share Zanzibar 28 Januari 2024: Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kutwaa mkanda wa WBO Africa Middle Weight kwa kumzibua ‘kumtwanga’ kwa KO, raundi ya 7 Bondia kutoka nchini Ghana, Elvish Ahorgah. Katika pambano hilo lililoanza kwa kasi kila mmoja akionesha kuuwania mkanda huo Mwakinyo aliweza kumnyamazisha kiaibu bondia huyo mwenye rekodi ya kutisha kimataifa. Pambano hilo lilipigwa uwanda wa ndani wa New Amaan Complex mjini Zanzibar usiku wa kuamkia leo. Kwa ushindi huo wa kishindo unamfanya Mwakinyo azidi kutisha hapa nchini na kuwapa hofu mabondia wanaojitapa kumtaka ulingoni. HABARI NA RICHARD BUKOS/ GPL 0 Share