The House of Favourite Newspapers

MWAKYEMBE AAGIZA MMILIKI WA GAZETI LA TANZANITE AHOJIWE

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe, amesema habari iliyochapishwa na Gazeti la kila siku la Tanzanite toleo la leo Jumatatu, Oktoba 29, 2018 lenye habari zenye tuhuma za kisiasa dhidi ya baadhi ya viongozi, haziakisi msimamo wa Serikali na ameagiza mmiliki na bodi ya uhariri ya gazeti hilo waitwe mara moja Idara ya Habari (MAELEZO) kujieleza kuhusu msingi wa habari hiyo.


Dkt. Mwakyembe amesema hayo leo mchana, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuelezea kushtushwa kwake na mwenendo wa gazeti hilo ambalo huchapisha habari zinazoibua tuhuma za kisiasa dhidi ya baadhi ya viongozi nchini, wakiwemo wabunge, wastaafu na kusababisha taharuki katika jamii.


Gazeti la Tanzanite linatolewa na kampuni ya CZ Information and Media Consultant LTD ya Dar es Salaam na leo katika toleo lake Na. 254 limeandika katika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa kinachosomeka “Vigogo 14 hatari kwa nchi watajwa” ambayo inawataja viongozi kadhaa wa kisiasa na wafanyabiashara.

Mwarabu asambaza picha za Diamond / Afungukia Safari zao!

Comments are closed.